Thursday, February 14, 2019


Jiwe la kiroho la kujengea na 8

 Imani ni nini?

 
 








Wabrania 11:1,“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, Ni bayana ya mambo yasionekana”.

Imani ni nini?
Imani ni kitu fulani ambacho kinafunuliwa kwako,ambacho hakijawa bado,lakini unaamini kitakuwa, Imani ni ufunuo wa mapenzi ya Mungu. Kwahiyo ni kwa ufunuo wa mapenzi ya Mungu. Kwahiyo ni kwa ufunuo (Waebrania 11.1)

Makanisa leo hayajaamini kwamba kuna ufunuo wa Kiroho, wanaamini juu ya mafundishio ya Mungu ya maungano ya utaratibu fulani. “Kwa ufunuo Habil alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora zaidi kuliko Kaini,ambayo Mungu aliishuhudia kuwa ni haki”. (Waebrania 11:4) Amen.
Natumaini unaliona hilo, Unaona mahali tunapoishi?
Unaona saa?

Nilikua nazungumza na Mungwana mmoja sio muda mrefu uliopita Mkristo msomi na muungwana alisema “Ndugu Branham tunakataa mafunuo yote” nikasema “Inabidi umkatae Yesu Kristo kwasababu yeye ni ufunuo wa Mungu, Mungu amefunuliwa katika mwili wa kibinadamu.
(1Timotheo3:16.),(Yohana 1:1-2,14) Mpaka utakapoliona hilo vinginevyo umepotea Yesu alisema “Msipoamini kwamba mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu
Yeye alikua ufunuo wa Mungu,yule Roho wa Mungu akijifungua katika umbo la kibinadamu, kama huezi ukaamini umepotea,ukimfanya yeye kuwa nafsi ya tatu,nafsi ya pili,au nafsi nyingine tofauti na Mungu umepotea, “Usipoamini kwamba mimi Ndiye, Mtakufa katika dhambi zenu”. Ufunuo [1]

Na ufunuo ni kitu cha pekee, Ufunuo wa Neno, Ule ufunuo wa Neno. Ufunuo ni nini?                                             
                                                                              1
Yesu alisema “juu ya mwamba huu mtalijenga kanisha langu na milango ya kuzimu haiwezi kulishinda (Matayo 16:13-20), Imani ni ufunuo, Kwasababu imani imefunuliwa kwako, Habil kwa imani alitoa Dhabihu kwa ufunuo (imani) kamtolea Mungu dhabihu ilio bora kuliko Kaini, Kaini alifikili kwamba wamekula matofaa, bado wanawazo hilo mpka leo ilikua ni uzinzi, uzao wa nyoka na pale mihuri saba ilipofunguliwa ililitangaza hilo na kulithibitisha, Angalia hilo ni lakimaandiko kutoka mwanzo mpka ufunuo [2].

Lakini Habil hakuja na muundo, lakini Kwa imani biblia ilisema alimtolea Mungu sadaka ilio bora zaidi kuliko Kaini na Mungu akashuhudia kuwa ni haki, Kwasababu aliona mpango wa Mungu ambao ulifunuliwa kwake……

Biblia wakati huo ilikuwa haijaandikwa, kwahiyo kama Kaini ambaye ni ndugu yake walikaa chini ya mafundisho ya baba na mama akaleta matunda kutoa sadaka.

Lakini Habil kwa ufunuo aliona kwamba haikua ni matunda yaliyo watoa Bustani ya Edeni kama watu wengine hufikiri hivyo hata leo. Haikua ni matunda ilikua ni damu ya mama yake aliyemfamya kuwa anayepatikana na mauti, au Baba yake, kwahiyo alikuja kutoa Dhabihu ya Damu ya mwanakondoo kwa ufunuo wa Kiungu (Mwanzo 4:1-7), Hakuna mtu yoyote aliyemwambia kitu chochote juu ya hilo, lakini yeye kwa ufunuo alimuona mwana wa Mungu akija, akitoa mwana wa Kondoo kwa mfano wa Kimbele, Akimuona Yesu kuwa ni mwana Kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya Ulimwengu (Ufunuo 13:8) , na Mungu alishuhudia “Hiyo ni kweli” Mungu siku zote alishuhudia ukweli, sasa Kaini alipoona ndugu yake Dhabihu yake imekubaliwa  alimuua ndugu yake kwasababu ya wivu [3]
                                                                                           2
Ondoka mbali na thiolojia zako na hisi zako mwenywe, muache tu Roho Mtakatifu….Ulipewa hisi tano, lakini hizo hisi tano ambazo ni za akili zako, kamwe hukupewa ili zikuongoze (Warumi 8:14, 1Wakorintho 2:13),Ila hisi ya sita ambayo ni imani,ulipewa hiyo ikuongoze wewe. Hivyo ni hisi ya sita na hiyo ni hisi kuu, Hiyo inakuongoza wewe [4].

Sasa angalia imani ni nini? Imani ni hisi ya sita. Hisi tano zina mtawala huyu mtu, Mungu alimpa mtu hisi tano Ili aweze kuwa na mawasiliano nyumbani kwake duniani, Huwezi kuwasiliana na Mungu kwa hisi zako tano, Unamjua Mungu kwa imani ambayo ni hisi ya sita. Kuna hisi mbili katika nafsi ,imani na kutokuamini na kama wewe umeshikiliwa na imani, Imani kwako ni kitu halisi kabisa kama vile kuona kulivyo halisi kama unaamini hilo shati ni jeupe, Kama una macho na unaimani kwa kuona kwako na unasema lile shati ni jeupe…Kama unaamini kwamba Yesu Kristo alikuponya pale Kalvari, na Imani yako inatangaza hilo  kwa kadri ya kuona kwako inavyo tangaza hili,Wewe unakuwa uliyeponywa, hapo hilo limekwisha. Unaona! Imani ni hakika ya mambo ya tarajiwayo bayana  ya mambo yasiyoonekana, Onja, Jisikie, kunusa au kusikia.Unaliamini hilo. Sema “Vema sisikii chochote cha tofauti” hupaswi kusikia chochote cha tofauti unapaswe kuamini [5].

Sio msisimko tu , Sio kitu cha kuwazia ni kitu halisi, kitu cha kweli kuona kutashindwa, kila kitu kingine kitashindwa. Lakini Imani haiwezi kushindwa, kwa sababu inaenda kwenye viwango vikuu zaidi ya mambo ya asili na haiwezi kushindwa.[6]

Sasa Imani “Ni ufunuo kutoka kwa Mungu”sasa imani ni ufunuo. Hapo ndipo ninapotaka kubaki hapo kwa muda mfupi,Ni ufunuo umelifanya hilo kwako kwa neema yake .
                                                                            3
Sio chochote ulichofanya, Siyo chochote ulicho tendea kazi wewe mwenyewe kuja kwenye imani.kamwe wewe ulikuwa huna imani, umepewa hiyo Kwa neema ya Mungu (Waefeso 2:8-9)

Mungu amelifunua hilo kwako,kwa hiyo imani ni ufunuo,Na kanisa lote la Mungu linajengwa kwenye ufunuo, katika kusanyiko la watu ambapo wanakuja kwenye mstari wa maombi,utaona wengine …. Na wote ni watu wazuri, na tuseme.Kuna wengine wanajitahidi sana kuamini hilo, Wakijalibu kujisukuma wenyewe katika hlo wengine hawawezi hivyo kabisa.

Wengine, ni kwa neema tu wanapewa hilo .Sasa hapo ndipo unaona tofauti,Unaona!
Hilo ndilo linalofanya Hilo, Huo ndio ufunuo kwa Mungu lazima ufunuliwe kwanza [7]

Lakini kwa kanisa yule Bibi harusi unyakua ni ufunuo kwake, unafunuliwa kwake, yule Bibi harusi wa kweli wakristo atakua akingoja ufunuo wa kunyakuliwa,sasa,Huo hi ufunuo kwa maana ufunuo ni imani, huwezi ukawa na ufunuo bila kuwa na imani,Huu ni ufunuo,kwasababu ni kitu fulani kinafunuliwa  kwako.Imani ni ufunuo.Imani kitu fulani ambacho kimefunuliwa kwako ilivyokuwa kwa Abrahamu ambaye aliita kitu kingine chochote kinyume na kile kilichofunuliwa kwake kwamba hakiko (Warumi 4:16-22),sasa imani,hiyo ndiyo imani ilivyo. Ufunuo wa Mungu, Kanisa linajengwa juu ya ufunuo ule mwili wote. [8]

Hapa kuna swali alilopewa nabii wa Mungu nataka kupokea roho mtakatifu, nataka kujua kinipasacho kufanya,nina mzigo wa kutaka familia yangu iokolewe? kama unataka kupokea Roho Mtakatifu, ngoja nikwambie kitu fulani:-Biblia inasema “wamebarikiwa wale walio na njaa na kiu ya haki”
(Matayo 5:6).
                                                                                     4

Wewe umebarikiwa sana kwakuwa na shauku kutaka hilo, unaona? Sasa kumbuka,sio kwamba umelipata hilo,lakini wamebarikiwa wenye njaa na kiu ya haki ya kutaka hilo, “kwamaana watajazwa” wewe kaa pamoja na hilo “ nifanye nini kwa ajilii ya familia yangu?” tumia imani hiyohiyo unayoitumia kwaajili yako mwenywe, kwaajili ya familia wakabidhi kwa bwana na uamini kwa moyo wako wote kwamba watu wataenda kuokolewa usiache hio ije katika akili zako za kawaida, iache iangukie kule ndani kwenye kilindi cha moyo, hapo sasa watakuwa ni wako, Mungu atakuwa amekupa wewe wawe wako inapoangukia chini kule,chochote ulichonacho katika moyo wako hapa na ukamueleza hilo, wakati unaomba amini kwamba unakipokea kile ulichoomba, (Mathayo 7:7-11) sasa hupaswi kulitilia shaka tena huwezi ukaliamini na ulitilie shaka wakati huo huo, inabidi uamini kile ulichoomba kwamba unakipokea hicho, hapo Yeye alisema hicho utapewa kwahiyo wewe amini kwaajili ya familia yako, nao watalipata hilo [9].

Kama unayo imani kwa ajili ya uokovu wako mwenywe, Je huwezi kuwa na imani ambayo itatenda kazi kwa watu wako? Imani ni nini? Ni nguvu isiyoonekana unaona? Ni roho
 (Wakorintho 2:4-13) Roho Mtakatifu analeta imani,unaona? Ni nguvu isiyoonekana  [10].

 Hiyo ndiyo nguvu iliyo ndani ya kanisa sasa. ( Wakorintho 2:4-7, Waefeso 1:11-23),Lakini inataliwa na sheria na hiyo sheria siyo sheria ya kushika amri, ni sheria ya imani, Yesu alisema “ Mambo yote yanawezekana kwake aaminiye” (Maiko 11:23-24). Kama unaweza kuliamini hilo, chochote Mungu atakachoongoza nafsi yako kuamini hicho ni chako.
                                                                      5

 Kila mahali unyayo wa mguu wenu utakapo kanyaga kwa imani Mungu anakupa utakapo kanyaga kwa
imani, Mungu anakupa hilo (Joshua 1:3) Amina, Hiyo ni yako unamiliki hiyo kama unaweza kupata ufunguo kwa hii sheria ya
imani ambayo inafungua hili kwako, unaona ninachomanisha? Hivyo nguvu inataliwa na …. Kama wewe ni mwana wa Mungu, ni binti wa Mungu, hilo halikuachi. Liko na wewe pamoja wakati wote, lakini imani yako inaenda mbali na hilo, Lakini bado lipo pale Haleluya? [11]

Na sasa Yesu ni mlango wa Mambo haya yote (Wakorintho 1:1:4-9), na imani ni ufunguo ambao unafungua mlango, sasa. Kama Yesu ni mlango kwa ahadi zote za Mungu, Imani katika kazi yake iliyokamilika inafungua kila mlango wa kila hazina iliyo ndani ya ufalme wa Mungu, unaona hilo? Imani ni ufunguo ambao unafungua kila ahadi aliyoahidi, Ufunguo wa Imani unafanya hilo katika kazi yake iliyokamilika. Ni hizi funguo ndizo tunazo zizungumzia [12].

Kila mmoja inabidi awe na kitu fulani ambacho una uhakika nacho, na hapo ndipo unaweza kuweka imani yako, ni pale unapokuwa na uhakika kama kuna swali liache hilo mpaka uwe na uhakika [13].
Fikiria tunayo nanga (Amina) tunayo Nanga ambayo ipo katika pazia. Hatuwezi kuiona hiyo wakati mwingine, Lakini unajua iko pale. Kama vile ambavyo kijana mvulana aliyekuwa anarusha tiara wanasema “Iko wapi?” akasema “siwezi kuiona hiyo” akasema “Najua bado ipo pale,kwasababu naweza kuisikia” kwahiyo ni kweli, tunaweza tusiwe na uwezo wa kuiona hiyo nyakati zinakuwa giza. Mawingu yanaweza kuficha uso wake uliobarikiwa kwa muda, Lakini kumbuka mawingu yanaweza yakaficha uso wake lakini hayawezi kumficha yeye yanaweza yakalificha
                                                                                      6
usilione lakini bado linawaka nyuma ya mawingu. Na imani inaliona jua kupita mawingu. Uzoefu mkubwa sana katika maisha yangu ni pale ninapokutana na mlima  uliyo kinyume na mimi ambao siwezi ni kuuvuka juu yake, chini yake , Au  kuuzunguka, Ninasimama nikitulia, Na Mungu alitusogezea  kitu hicho nyuma. Haijalishi kuna giza la  mawingu kiasi gani, Imani  inapenya ng’ambo na jicho ambalo linaangalia nyuma ya kitu ambacho SHETANI amekiweka mbele yako, Kwasababu Mungu ni ushindi wetu Ameni, hata kifo chenyewe hakikutii hofu sio ajabu, Mwaminio anaweza akasimama na kusema : ooh Kifo uko wapi uchungu wako na kaburi, uko wapi ushindi wako lakini shukrani kwa Mungu anayetupa ushindi kupitia bwana wetu Yesu Kristo”
 ( 1 wakorintho 15:51-58) Hiyo ndiyo imani inayotufanya tusione aibu, Hiyo ndiyo imani inayoshinda         [3].
Imani ni nini? Watu wengi wanaweka tumaini badala ya imani lakini hayo ni mambo tofauti sana kama vile mchana na usiku kwasababu Biblia katika (Waebrania 11:1) imesema “ Imani ni hakika ya mambo tarajiwayo bayana ya mambo yasioonekana” sio tu tumaini hakuwazia, ni kitu cha uhakika oh natumaini mnaliona hilo, na hapo sasa utaona mambo ya kitendeka unaona? Watu wengi wanaweza wakawa na tumaini katika mawazo ya akili zao nasikitika kusema hili,hiyo ndiyo sehemu kubwa ya wakristo wengi wanaojiita hivyo ni mawazo ya kufikiria wana wazo fulani lakini hawana uzoefu kamwe wa kile Yesu alichosema “ Mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme” au lile neno lililotafsriwa kwa usahihi ni kuelewa ufalme wa Mungu ( Yohanna 3:3). Unaangalia kitu chochote unasema “hicho sikioni” humaanishi kwamba hukioni na macho yako, hukioni na moyo wako, hukielewi.
Sasa kuna vitu viwili ambavyo vinamfanya mwanadamu, kimoja ni akili yako na kingine ni nafsi yako na akili ni mawazo ya ubongo wako, uelewa wako, na nafsi yako ni sehemu ya Mungu ambayo
                                                            7
 ipo ndani yako, unapozaliwa duniani kama mtoto, unakuwa nafsi iliyo hai (ishiyo)na unafikia umri wa kuchagua,unasikia injili kwa njia ya masikio, kuna kitu fulani ndani yako kinakuwaambia mpokee Kristo utasema “ Vyema mimi bado ni mdogo na tusubiri muda kidogo” sasa hapo ndipo unafanya kosa lako la kwanza hapo, kwasababu unamhuzunisha huyu mtu wa ndani. Mungu hataenda kukuhukumu wewe kwa huyu mtu hapa wa akili zako. Ataenda kukuhukumu wewe kwa nafsi yako.  Watu wengi wana imani kwa akili zao, wengine wana imani kwa nafsi zao sasa, zile akili hapa zitahojiana na neno la Mungu “Zitaona siyo za kibusara” lakini nafsi haina hoja yeyote inasema “hilo ni kweli”. Na hiyo inamaliza yote.  Unaona, nafsi ina amini hilo.  Akili zitasema “Nashangaa linaweza likawa siku zilizopita.  Hilo linaweza likawa kwa ajili ya wanafunzi au likawa kwa ajili ya kitu fulani.  Siyo kwa ajili yetu sasa kwa sababu tunaishi katika siku tofauti” lakini nafsi inasema “Kristo ni Yule jana, leo na hata milele”.  (Waebrania 13:8), hakuna hoja, haina hoja hata kidogo.  Inaamini.  Sasa, sehemu kubwa ya sisi, marafiki, tutaenda kuhoji badala ya nafsi na hiyo ndiyo sababu tunashindwa kupata Baraka za ajabu kutoka kwa Mungu, sasa hiki sio kitu chakuwazia tu kitu fulani, siyo kitu cha kichawi.  Ni kweli neno la Mungu.                    [14]

Sasa imani inateka, imani ni ushindi (1Yohana 5:4).  Sio tu mtengeneza imani, inashinda, Imani ni ushindi ambao unaishinda Dunia, inafanya nini? Imani ni nini? Imani ni mtekaji? Kuteka na kushinda ni jambo lilelile.  Kuteka inamaanisha kumpiga na kummaliza, kumzidi, kumzuia, kumtia jela, kumtupa gerezani, inamaanisha hivi ile dhambi ambayo ilikutawala wewe sasa unaitawala, (Warumi 5:17-21) ina maana kwamba wewe umeshinda hili, umelichapa hilo, wewe ni mkuu kuliko hilo, Najisikia wa kidini, najisikia wakidini sasa hivi.  Nani alikuwa wa kwanza?
                                                                                     8

 Mwenye dhambi au mkombozi?
 Mkombozi kwa sababu Mkombozi ana nguvu kuliko dhambi.  Ni kipi cha kwanza uponyaji au magonjwa, haingekuwa mponyaji ila ingekuwa juu ya magonjwa. Ni mponyaji, kwa sababu unaweza kushnda magonjwa.  Na imani ni ushindi unao shinda kila laana ya shetani. Imani ni ushindi.        [15].
Imani ni nini? Imani ni kweli, imani ni kitu fulani ambacho unakijua kwa uhakika, imani siyo kitu ambacho una bahatisha.  Imani ni kitu ambacho unajua, kitu fulani ambacho kinakuja chini ndani ya nafsi yako.      [16].
 Unaweza ukawa na vikwazo vingi.  Pengine daktari wako anasema haiwezi kutokea Lakini kama una imani haifanyi tofauti mtu mwingine anasema nini.  Imani yako haizuiliki, Imani haina ya kunuia, Imani inaliona Hilo                   [17].

 Sasa kuna vitu vitatu ambavyo watu wanaishi kwa hivyo,moja kitu kile cha kibinadamu,pili ufunuo wa kiungu na tatu ni maono,unapoomba na mtu yoyote kwa kwa namna ya kibinadamu tunasema “vema na tumaini utapata  nafuu.unaona,ninatumaini pamoja  na wewe, najalibu kutumia imani yote niliyo nayo” Hicho ni cha kibinadamu, pili  ni ufunuo wa kiungu kitu fulani kinapo funuliwa kwako, unajua tu moyoni mwako hicho kitaenda kutokea na bado hakuna kitu chochote ni ufunuo tu,na tatu niono kwasababu hilo ni hii ASEMA BWANA,hiyo ni kamilifu na ya uhakika  [18].

Imani yako ya kiakili inaweza ikaamini vizuri, lakini ni mpaka imani ya Mungu iwe chini kule moyoni mwako __ _ _   (Wagalatia 2:19-20)
                                                                               9
Unaona,imani yako  ya kiakili inaweza ikalikubali, kufanya hivyo. Nakuendelea kuamini hilo kwa moyo wako wote mpaka Mungu alifunue hilo [7].
Sikiliza ninaenda kusema kitu fulani, angalia, imani haitambui, Amen,unaamini hilo? nimejifunza hilo katika miaka ya kutembea  sehemu mbalimbali Duniani,nikikutana  na watu wa aina mbalimbali, lakini imani haijitambui unayo imani lakini wala hujui hilo hiyo ni kweli, YESU  KRISTO haijalishi  kama alikuwa kwenye  Dhoruba na mawimbi yakipiga kutoka upande mmoja wa mtumbwi hadi mwengine au akiwa amesimama katika uso wa vurugu za mapepo, hata kama angekuwa amending’inia mahali fulani  hiyo haikumsumbua Yeye,Yeye alitembea kwa utulivu na kwa kimya kadri awezavyo Yeye kwa kirahisi alikuwa hatambui hofu au chochote kumzunguka yeye, hiyo ni kweli kama litaenda kutokea au kama haliendi kutokea alijua kwamba litaenda kutokea kwasababu Mungu alisema hivyo.Yeye hakusema  “ooh nashangaa  kama niliomba kikamilifu nashangaaa kama nilifunga muda mrefu wa kutosha, Nashangaa kama nilifanya kweli” Yeye alitembea akiwa hana fahamu, Hiyo ni sawa, Aliamini alichofanya Mungu kilikuwa kweli maandiko ilibidi yatimize na alijua maisha yake yatatimiza  hayo hivyo ni sawa, Na wewe uko hapa kuyatimiza pia tembea ukiwa huna fahamu za hofu, Tembea huna fahamu za kulaumiwa , Tembea ukiwa huna fahamu za Dunia, Tembea kama unatembea ndani ya Kristo. (Wagalatia 5:16-25) Tembea pamoja naye, usisikilize chochote cha mkono wa kuume wala wakushoto wewe endelea kusonga mbele, Kama kitu fulani kikija kanisani Tembea na Mungu, Haleluya!! Kama magonjwa yakikupiga wewe, Tembea Na Mungu, Kama majirani hawakupendi wewe tembea na Mungu, Endelea tu kutembea na Mungu, Enock siku moja alitembea pamoja na Mungu, unajua alichofanya?
   
                                                                                              10

 Alitembea njia yote kwenda nyumbani pamoja na Mungu. Alienda mbali sana na barabara hakutaka tena kurudi nyuma Amen!! (Mwanzo 5:22, Waebrania 11:5)     [19].












NUKUU ZA KINGEREZA
1.Wapakwa mafuta wa siku za maisha (65-072M) aya53-55
2. Muungano wa siri wa bibi harusi wa Kristo (65-1125) Aya 160-162
3.Nguvu ya Mungu (55-1006) Aya E- 14-E16
4.Mlango kuelekea kwenye Moyo (60-0605) Aya E-36
5. Mwanzo wa umaarufu wa Yesu (53-0605) Aya E-29
6.Kufufuliwa kwa binti yairo (54-0302) Aya E-13.
7. Imani ni matendo yaliyodhihirisha (65-1126) Aya 105,117,327
8. Unyakuo (65-1204) Aya 65-66
9. Maswali na majibu (640830M) COD UK.189 Swali no333
10. Maswali na majibu (64-0823M) COD UK 960,Aya 179
11. Maji yasiyo kama kutoka katika kwamba Mwamba (61-0723M) Aya 151
12.Ufunguo wa kwenye mlango (62-10007)
13.Kile kitendawili (65-0117) Aya 16
14.Yesu Kristo Yule jana na hata milele (55-0806) Aya E16_E18
15.Imani ni ushindi wetu (58-1004) Aya E-23
16.Sura za Kristo (59-0525) Aya E-23
17.Kun’ang’ania (62-0719E) Aya E56
18 Ile satina (55-0522) aya 6
19 Aliapa kwa nafsi yake (54-1212) Aya 101-104